Kuomba pesa ya kodi kabla ya wakati wake

Swali: Kuna mahali nakodi na anakuja yule mtu aliyenikodishia na anataka kodi kabla ya kutimia muda wa kulipa kodi na kunambia nilipe kodi na kwamba ataniondoshea Riyaal 500. Je, inajuzu kufanya hivo?

Jibu: Mtu huyu anasema kwamba amekodishiwa duka au nyumba kwa pesa 5000. Katikati ya mwaka anakuja mwenye nyumba au duka kwamba ampe 4000 na atamwaondoshea 1000. Je, inauzu au haijuzu? Inajuzu na hakuna ubaya kufanya hivo. Kwa sababu ndani yake kuna manufaa kwa pande zote mbili.

Vivyo hivyo kwa mfano mtu anadaiwa 100.000 na amepangiwa muda wa kulia ni miaka kumi ambapo kila mwaka analipa 10.000 Mwenye deni lake akamwambia naomba hivi sasa unipe 5.000 na pesa ya kubaki nakuangushia nayo, inafaa kufanya hivo kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu. Kwa sababu kitendo hichi kina manufaa kwa pande zote mbili. Isitoshe ndani yake hakuna ribaa. Bali kuna upungufu kinyume na ribaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1305
  • Imechapishwa: 23/10/2019