Kuomba Mambo Ya Kidunia Na Aakhirah Katika Swalah Ya Faradhi


Swali: Je, inajuzu kuomba Du´aa katika Swalah ya faradhi kwa kitu katika mambo ya kidunia kama kwa mfano kusema “Ee Allaah! Ninakuomba mali, nyumba au mengineyo” katika mambo ya kidunia?

Jibu: Kuishia kuomba dunia haijuzu. Wanasema kuwa hili linabatilisha Swalah. Ama akijumuisha katika Du´aa yake baina ya dunia na Aakhirah, hili halina neno. Hili ni jambo zuri:

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Mola wetu Tupe katika dunia mema na katika Aakhirah (pia Tupe) mema na Tukinge na adhabu ya Moto.” (02:201)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014