Kuomba mambo ya kidunia na Aakhirah katika swalah ya faradhi

Swali: Je, inajuzu kuomba du´aa katika swalah ya faradhi kwa kitu katika mambo ya kidunia kama kwa mfano kusema “Ee Allaah! Ninakuomba mali, nyumba au mengineyo” katika mambo ya kidunia?

Jibu: Kuishia kuomba dunia haijuzu. Wanasema kuwa hili linabatilisha swalah. Ama akikusanya katika du´aa yake kati ya dunia na Aakhirah, hili halina neno. Hili ni jambo zuri:

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Mola wetu Tupe katika dunia mema na katika Aakhirah pia Tupe mema na tukinge na adhabu ya Moto.” (02:201)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014