Kuomba kwa du´aa nyingine katika swalah kwa yule asiyejua du´aa ya maiti

Swali: Ikiwa mtu hajui Du´aa zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuombee maiti kwa Du´aa anayoweza?

Jibu: Ndio. Amuombee maghfirah na rahmah. Haya kila mtu anayaweza na himdi zote ni za Allaah. Amuombee maghfirah na rahmah na kumuokoa na Moto.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014