Kuomba kunyweshelezewa katika du´aa ya Qunuut

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma kwa kuremba sauti du´aa ya Qunuut? Ni ipi hukumu ya kuomba kunyweshelezewa katika du´aa hiyo?

Jibu: Ikiwa muulizaji anamaanisha yule msomaji wa Qunuut kusimama katika kila sentesi ya du´aa ni sawa ili waswaliji waweze kuelewa kwa uzuri kile kinachosemwa na imamu wao na kuitikia “Aamiyn”. Ama ikiwa anaisoma kwa njia ya nyimbo haifai na haiwezekani. Watu hawana haja ya kuyasikia maneno yako kama nyimbo. Wao wako na haja ya du´aa watayomuomba kwayo Allaah (´Azza wa Jall).

Ama kuhusu kuomba kunyweshelezewa hakuna neno mtu akaomba kunyweshelezewa katika du´aa y Qunuut. Kwa sababu du´aa ya Qunuut ni du´aa isiyofungamana. Kunatakiwa kutajwa yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Zaidi ya hapo mtu ana khiyari ya kusoma atakacho.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1600
  • Imechapishwa: 30/05/2018