Kuomba kuharakishiwa jambo katika du´aa

Swali: Ni ipi hukumu ya muombaji kuomba kufanyiwa mbio mahitajio yake kama kwa mfano kusema “Ee Allaah! Niharakishie faraja au kadhaa?”

Jibu: Ikiwa ametenzwa nguvu hakuna neno akamuomba Allaah amharakishie. Ama ikiwa hakutenzwa nguvu amuachie mambo Allaah (´Azza wa Jall). Huenda kucheleweshewa kwake ni bora kuliko kuharakishiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montaqo-17-10-1434_1.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020