Kuomba du´aa ya kinga kabla ya Tasliym

Swali: Kuomba du´aa ya kujikinga na mambo mane “Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kinga dhidi ya adhabu ya kaburi… “ mpaka mwisho kabla ya Tasliym. Je, ni wajibu au imependekezwa?

Jibu: Imependekezwa. Imependekezwa na sio wajibu. Kwa kuwa wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomfunza mwenye kuswali vibaya katika swalah yake namna atakavyoswali hakumfunza jambo hili, haya ni mambo ambayo yanaikamilisha swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014