Kuomba Du´aa Ya Kinga Kabla Ya Kutoa Salaam


Swali: Kuomba Du´aa ya kujikinga na mambo mane “Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kinga dhidi ya adhabu ya kaburi… “ mpaka mwisho kabla ya kutoa Salaam. Je, ni wajibu au imependekezwa?

Jibu: Imependekezwa. Imependekezwa na sio wajibu. Kwa kuwa wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomfunza mwenye kuswali vibaya katika Swalah yake namna atakavyoswali hakumfunza jambo hili, haya ni mambo ambayo yanaikamilisha (kuipamba) Swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014