Swali: Je, kuna du´aa maalum kwa ajili ya kukhitimisha Qur-aan? Ni upi sahihi wa du´aa inayonasibishwa kwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)?

Jibu: Hakukupokelewa dalili inayolengesha du´aa maalum kutokana na ninavojua. Kwa ajili hiyo inafaa kwa mtu kuomba du´aa ya yale anayotaka na achague katika zile du´aa zenye manufaa kama mfano wa kuomba kusamehewa madhambi, kufuzu kwa Pepo, kuokoka kutokamana na Moto, kujilinda kutokamana na fitina, kuomba mafanikio ya kufahamu Qur-aan tukufu kwa njia inayomridhisha Allaah (Ta´ala), kuitendea kazi na kuihifadhi na mfano wa hayo. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alikuwa akiwakusanya familia yake wakati anapokhitimisha Qur-aan na akaomba du´aa.

Kuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukupokelewa chochote katika hayo kutokana na ninavojua.

Kuhusu du´aa inayonasibishwa kwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) sijui usahihi wa kunasibishwa kwake. Lakini ni du´aa iliyotangaa kati ya Mashaykh wetu na wengineo. Lakini mimi sijaliona hilo katika chochote katika vitabu vyake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/358)
  • Imechapishwa: 06/11/2021