Swali: Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa kwenye makaburi ya mawalii kwa lengo la kuitikiwa du´aa?

Jibu: Hii ni miongoni mwa Bid´ah. Kuomba du´aa na kuswali karibu na makaburi ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki. Sunnah ni mtu atembelee makaburi, awatolee salamu na awaombee du´aa kisha aondoke. Kama anataka kujiombea du´aa mwenyewe basi jiombee maeneo mengine. Kuomba du´aa, kusoma Qur-aan na kuswali maeneo ya makaburi ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki na ni miongoni mwa Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 14/11/2021