Kuomba du´aa baada ya kumaliza kukimu swalah

Swali: Nimegundua baadhi ya waswaliji pindi muadhini anapomaliza kukimu swalah basi hunyanyua mikono yao na huomba du´aa na hayo wanayafanya kabla ya Takbiyrat-ul-Ihraam. Je, haya yamepokelewa au hapana?

Jibu: Hayana msingi. Haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa anaomba kitu baina ya adhaana na Iqaamah. Wala haikuhifadhiwa kutoka kwake kwamba alinyanyua mikono katika maeneo haya. Bali haitakikani kwa yeyote kufanya hivo. Ni kitendo kinachokwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/346)
  • Imechapishwa: 19/09/2021