Kuoga kwa sababu ya ijumaa kunamtosheleza mtu na kutawadha?

Swali: Kuna mtu ameoga ghuslu ya ijumaa na akaswali pamoja na mkusanyiko pamoja na kwamba hakutawadha wudhuu´ kwa ajili ya swalah. Alikumbuka kuwa hakutawadha baada ya kuoga alipokuwa katikati ya swalah. Je, swalah yake ni sahihi au ni lipi la wajibu kwake ikiwa swalah yake si sahihi pamoja na kuwa kumeshapita wakati mrefu?

Jibu: Ni lazima kwake kuirudi hiyo swalah na badala yake aswali Dhuhr. Kwa sababu kuoga kwa ajili ya ijumaa hakutoshelezi mtu kutohitajia wudhuu´. Ni lazima kwa mtu atie wudhuu´ wa Kishari´ah. Lakini endapo itakuwa ni kuoga kwa ajili ya janaba na mtu akanuia kuondosha hadathi zote mbili ni sahihi[1]. Ama kuhusu kuoga kwa ajili ya ijumaa hakutoshelezi. Bali ni wajibu kwake badala yake arudi kuswali Dhuhr. Kwa sababu ijumaa inapokidhiwa inakuwa kwa mtindo wa Dhuhr.

Swali: Kwa hiyo kuoga kulikopendekezwa hakutoshelezi kutokamana na wudhuu´ hata kama mtu atanuia?

Jibu: Hakutoshelezi kutokamana na wudhuu´ isipokuwa atapopangilia; akaanza kuoga uso, mikono, akaosha kichwa chake kukiwemo masikio kisha akaosha miguu yake kipindi yuko anaoga. Akifanya hivi ni sawa na kunatosheleza.

Muulizaji: Hivi ni kama ametawadha?

Jibu: Ndio. Anatawadha na wakati huohuo yuko anaoga. Anatakiwa kufanya kwa kupangilia na kunuia.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuoga-kwa-sababu-ya-jua-kali-kunamtosheleza-mtu-na-kutawadha/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/noor/7967
  • Imechapishwa: 14/11/2017