Kuoga kwa ajili ya ijumaa usiku wa alkhamisi II

Swali: Nikiwa niko na janaba na nikaoga siku ya ijumaa – je, josho hili linatosha kutohitajia kuoga josho la ijumaa au natakiwa kuoga josho lingine? Je, inasihi muislamu akioga usiku wa kuamkia ijumaa?

Jibu: Mtu akioga usiku wa kuamkia ijumaa haitoshi kutokamana na josho la ijumaa. Ama akioga siku ya ijumaa kwa ajili ya janaba basi inatosheleza kutokamana na josho la ijumaa. Ni kama ambavyo swalah ya faradhi inatosheleza kutokamana na Tahiyyat-ul-Masjid. Hapa mtu ameoga josho lililowekwa katika Shari´ah – ambalo ni josho la janaba – na likamtosheleza kutokamana na josho lililowekwa katika Shari´ah siku ya ijumaa. Lakini endapo mtu katika josho moja atanuia josho zote mbili ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1546
  • Imechapishwa: 17/05/2019