Kuoga kunamtosheleza mtu na kutawadha?

Swali: Kuna mtu ameoga pasi na kutawadha. Je, inatosha kufanya hivo?

Jibu: Bora ni yeye kutawadha kisha aoshe/aoge sehemu ya mwili wake uliobaki[1], kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivokuwa akifanya. Endapo atakomeka na kuoga peke yake pasi na kutawadha ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye kujulikana kwa madhehebu ya maimamu wanne. Lakini Abu Haniyfah na Ahmad wanaonelea kuwa ni wajibu kupalizia na kusukutua. Upande mwingine Maalik na ash-Shaafi´iy wanaonelea kuwa sio wajibu kwake kufanya hivo. Je, anuie kuondosha hadathi? Wanachuoni wametofautiana juu ya hili. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuoga-kwa-sababu-ya-jua-kali-kunamtosheleza-mtu-na-kutawadha/

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/297)
  • Imechapishwa: 14/11/2017