Kuoga josho la ijumaa baada ya alfajiri

Swali: Vipi mtu akioga josho la ijumaa usiku au baada ya alfajiri na akanuia kuwa ni josho la ijumaa?

Jibu: Akioga kabla ya alfajiri hainufaishi kitu. Kwa sababu hapana shaka kwamba siku haijaingia. Akioga baada ya alfajiri inaweza kufaa. Lakini bora ni yeye kuoga baada ya jua kuchomoza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13370
  • Imechapishwa: 27/09/2020