Kuoa zaidi ya mke mmoja kunajuzu pale mume anajiamini uadilifu

Swali: Tunaomba uzungumzie juu ya kuoa wake wengi na vipi mwanaume atangamane na wake zake?

Jibu: Mwanaume akiwa na wake wengi basi ni wajibu kwake kufanya uadilifu kati yao katika mambo mane:

2- Kumlisha.

2- Kumvisha.

3- Nyumba.

4- Kumgawia siku sawa. Kila mmoja awe na siku yake hata kama atakuwa na hedhi au nifasi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya uadilifu kati ya wake zake na akisema:

“Ee Allaah! Hili ndio ninaloliweza na usinilaumu kwa unachokimiliki Wewe na si mimi mwenye kukimiliki.”

Kuoa wake wengi kunajuzu ikiwa mwanaume anajiamini kama atakuwa mwadilifu. Ikiwa hajiamini haijuzu kwake kufanya hivo. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne. Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi [bakini na] mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea [udhulumu].” (04:03)

Kufanya uadilifu kati ya wanawake inakuwa katika mambo haya mane; matumizi, mavazi, nyumba na kumgawia siku sawa.

Kuhusiana na mapenzi ya moyoni na zile hisia anazohisi, hiki ni kitu asichokimiliki mtu. Hivi ndivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akifanya uadilifu na kusema:

“Ee Allaah! Hili ndio ninaloliweza na usinilaumu kwa unachokimiliki Wewe na si mimi mwenye kukimiliki.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.islamway.net/lesson/138827/%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%AD%D9%82%D9%88%D9%82-%D9%88%D9%88%D8%A7%D8%AC%D8%A8%D8%A7%D8%AA?ref=s-pop
  • Imechapishwa: 24/09/2020