Kuoa Sio Kikwazo Cha Kumzuia Mwanafunzi Na Kusoma


Swali: Kuoa kunamzuia mtu na kutafuta elimu? Vijana wengi wanaume na wanawake wanatumia hoja hiyo. Ni yapi maoni yako kwa mwanafunzi anayesoma kwenye chuo kikuu?

Jibu: Ikiwa mtu yuko na uwezo basi kuoa sio kikwazo kinachomzuia mtu na kutafuta elimu. Ni kweli kwamba inaweza ikawa ni kizuizi endapo mtu atakuwa hana uwezo na akachelea ikiwa ataoa itampelekea katika kuoa matumizi ambayo hawezi kuyamudu na wakati huo huo huku anatafuta elimu. Katika hali hii hapa ndipo inaweza kuwa kikwazo. Pamoja na hii hali sisi hatumkati tamaa kijana ya kuoa. Tunamwambia: oa na Allaah (Subhaanahu wa Ta?ala) atakutajirisha wewe na ahli wako. Imekuja katika Hadiyth:

“Kuna watu aina tatu ni haki kwa Allaah kuwasaidia” ambapo akataja mmoja wao kuwa: “Ni yule mwenye kuoa ambaye anataka kujisitiri.””

Kwa hivyo oa hata kama utakuwa mwanafunzi. Huenda kuoa kwako ikawa ni sababu ya kufunguliwa riziki yako kama ilivyoshuhudiwa kwa baadhi ya watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (12)
  • Imechapishwa: 28/05/2017