Kuoa ni wajibu au sunnah kwa mtazamo wa Uislamu?

Swali: Je, kuoa ni faradhi au sunnah?

Jibu: Kuoa ni sunnah iliyokokotezwa kwa yule mwenye kuweza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule atakayeweza miongoni mwenu kuoa basi na aoe. Hakika hilo linamfanya ainamishe macho na inahifadhi utupu wake. Yule asiyeweza basi ni juu yake afunge. Kwani kwake ni kinga.”[1]

Kwa baadhi ya watu inaweza kuwa faradhi kukikhofiwa juu yao fitina ya kutumbukia katika machafu na wakati huohuo wako na uwezo wa kuoa.

[1] al-Bukhaariy (1905), Muslim (1400), at-Tirmidhiy (1081) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/07)
  • Imechapishwa: 11/06/2017