Swali: Ipi hukumu ya kuandika Aayah maalumu za Ruqyah kama al-Faatihah na nyinginezo (katika karatasi) na kuweka kwenye maji ya zafarani akikususudia kukoga na kunywa maji hayo mgonjwa? Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Hili limeruhusiwa na baadhi ya Salaf, kama alivyosema Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “Zaad al-Ma´aad” na “at-Twib-un-Nabawiy”. Kasema ya kwamba, baadhi ya Salaf walikuwa wanafanya hivi, kwa kuwa hili linaingia katika Ruqyah ya Kishari´ah. Atakayefanya hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Q_VOJmGyikw
  • Imechapishwa: 25/03/2018