Swali: Je, imewekwa katika Shari´ah kwa mgonjwa kuandika Aayah zinazohifadhi dhidi ya maradhi kwenye karatasi kisha akaziweka ndani ya maji? Na je, hili limethibiti katika Sunnah?

Jibu: Ndio, inajuzu kuandika Aayah za Qur-aan kwenye karatasi safi au kwenye sahani safi na kwa kalamu safi, kisha ioshwe (hiyo Qur-aan) na kunywa. Mgonjwa ndio atakunywa. Hili limefanywa na Salaf na wanachuoni wameliruhusu. Kwa kuwa linaingia katika kujitibu kwa Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=8IYWzCbRS00
  • Imechapishwa: 24/03/2018