Swali: Je, anapata dhambi yule ambaye ataielekeza miguu yake kuuelekea msahafu kwa kukusudia au pasi na kukusudia? Tumesikia kuwa Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anamkufurisha mwenye kufanya hivo kwa makusudi. Je, haya ni kweli?

Jibu: Ikiwa malengo yake ya kuelekeza ni kuyadharau maneno ya Allaah basi anakufuru kwa lengo hilo. Lakini ambaye anafanya hivo pasi na kukusudia au anafanya hivo ili ajipumzishe basi huyo hakukusudia na hivyo hakufuru.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 20/03/2021