Swali: Je, kukata kucha baada ya Wudhuu na kunyoa ndevu kunavunja Wudhuu au hapana?

Jibu: Kukata kucha hakutengui Wudhuu, hali kadhalika kunyoa ndevu na kichwa. Kunyoa kichwa hakuvunji Wudhuu na wala sio katika mambo yanayovunja Wudhuu. Lakini kunyoa wala kupunguza ndevu haijuzu. Kwa kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Punguze masharubu na zirefusheni ndevu, mjitofautishe na washirikina.” Na anasema (´alayhis-Swalaat was-Salaam): “Punguzeni masharubu na zirefusheni ndevu mjitofautishe na Majuus (waabudu Moto).” Kasema: “… zirefusheni ndevu.” Kaamrisha (´alayhis-Swalaat was-Salaam) kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu na kuzifuga. Haijuzu kwa Muislamu kuzinyoa wala kuzipunguza, kamwe. Badala yake, ni wajibu kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu na kuzifuga. Kwa kuwa, katika kufanya hivyo kuna kwenda kinyume na washirikina na kushikamana na mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuna kujitofautisha na wanawake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018