Kunyanyua na kupeana mikono baada ya swalah hayana msingi

Swali: Mara nyingi tunaona baadhi ya wenye kuswali pale ambapo imamu anapomaliza kutoa Salaam wanasalimiana wa kuliani na wa kushotoni na wanasema “Taqabbala Allaah” au “Haraman”. Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Hili halina asli. Kupeana mikono baada ya imamu kutoa Salaam ni jambo halina asli. Akitoa Salaam aseme “Astaghfiru Allaah” mara tatu kisha aseme “Allaahumma antas-Salaam, wa minkas-Salaam, Tabaarakta yaadhal Jalaali wal ikraam.” Kisha aseme “Laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka lah, lahul-Mulku walahul-Hamdu wahuwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr” mara mbili au akariri hilo mara tatu. Kisha aseme “Laa hawla walaa Quwwata illa billaah, laa ilaaha illa Allaah, wa laa na´abudu illa iyyaah, lahu ni´imatu walahul fadhwlu, wa lahuth-Thanaaul-husna, laa ilaaha illa Allaah, mukhliswiyna, lahud-Diyna walau kariyhal kaafiruun. Allaahumma laa maani´ limaa a´atwayta, wa laa mu´twiya limaa maana´ata, wa laa yanfau´ dhal jaddi minkal jaddi.”

Haya ndiyo yamesihi kutoka katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imependekezwa baada ya Maghrib na al-Fajr kuzidisha kwa kusema:

“Laa ilaaha illa Allaah wahdahuu laa shariyka lah, lahul-Mulku, walahul-Hamdu wahuwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr” mara kumi. Baada ya Maghrib na baada ya al-Fajr azidishe hili. Kisha alete Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr kila moja mara thelathini na tatu. “Subhaana Allah”, “Walhamduli Allaah” na “Allaahu Akbar” kila moja mara thelathini na tatu baada ya Swalah tano. Kisha amalizie kwa kukhitimisha mia kwa kusema “Laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka lah, lahul-Mulku walahul-Hamd, wa huwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr”. Haya yamependekezwa [Mustahab] baada ya kila Swalah tano. Kisha asome “Ayaat-ul-Kursiy”. Kisha asome “Qul huwaAllaahu Ahad” na “Suurat-ul-Falaq na an-Naas. Baada ya Maghrib na al-Fajr akariri mara tatu, mwanzoni mwa mchana na mwanzoni mwa usiku: Qul A´udhubi Rabbil-Falaq, Qul huwallaahu ahad na Qul A´udhubi Rabbin-Naas mara tatu [kwa kila moja].

Ama kunyanyua mikono baada ya Swalah hili halina asli, sawa kwa imamu wala maamuma wasinyanyue mikono yao wakitoa Salaam. Hali kadhalika baada ya Naafilah aseme “Astaghfiru Allaah” mara tatu, “Allaahumma antas-Salaam, waminkas-Salaam, Tabaarakta yaadhal Jalaali wal ikraam.” Lakini lau atanyanyua mikono baada ya (Swalah za) Naafilah katika baadhi ya nyakati hakuna neno. Imesimuliwa ya kwamba baadhi ya nyakati alinyanyua katika Swalah za Naafilah. Ama katika Swalah za faradhi hapana, ni jambo halikuwekwa.

  • Mhusika: Imaaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12796
  • Imechapishwa: 20/11/2014