Kunyanyua mikono wakati wa Tasliym


Swali: Wako waislamu ambao pindi wanapotoa salamu wanainua kidogo mkono wa kuume upande wa kuume kisha anapotoa salamu upande wa kushoto anainua kidogo mkono wake wa kushoto upande wa kushoto. Je, jambo hili linahusiana na dini?

Jibu: Jambo hili lina msingi, lakini hata hivyo alilikataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walipokuwa wanatoa salamu wanaashiria kwa mikono yao upande wa kulia na upande wa kushoto na wanainyanyua. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia:

“Ni kwa nini mnaashiria kwa mikono yetu kana kwamba ni mikia ya farasi ilio na wasiwasi?”[1]

Kisha akawabainishia kwamba inamtosha mmoja wao kutoa salamu upande wa kulia na upande wa kushoto kwa kusema:

السلام عليكم ورحمة الله

”Amani na rehema za Allaah iwe juuyenu.”

السلام عليكم ورحمة الله

”Amani na rehema za Allaah iwe juuyenu.”

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/108-tasliym/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (12) http://binothaimeen.net/content/6766
  • Imechapishwa: 23/01/2021