Kunyanyua mikono ni katika sababu za kupokelewa du´aa

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono katika Qunuut ndani ya Swalah?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo. Kunyanyua mikono wakati wa kuomba Du´aa ni katika sababu za kupokelewa Du´aa na ni katika adabu za Du´aa. Unamnyanyulia mikono Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014