Kunyanyua mikono katika du´aa


Swali: Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa kwa kunyanyua mikono baada ya swalah ya sunnah?

Jibu: Kunyanyua mikono katika du´aa ni Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akinyanyua mikono yake, katika swalah za sunnah na nyenginezo. Hata hivyo asinyanyue mikono baada ya swalah za faradhi. Ama baada ya swalah za sunnah hakuna neno kama tulivosema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017