Kunyanyua mikono juu katika wakati wa kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa

Swali: Khatwiyb akiketi juu ya mimbari siku ya ijumaa na muadhini akaadhini unaanza wakati wa kuitikiwa du´aa. Je, ambaye ananyanyua mikono yake juu wakati adhaana inatolewa akatazwe?

Jibu: Ndio. Aelezwe kwamba hakuna dalili ya kunyanyua mikono juu wakati adhaana inatolewa. Ni jambo halina dalili. Mikono hainyanyuliwi katika ule wakati wa kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa. Hakuna dalili juu ya hilo. Aomba pasi na kunyanyua mikono juu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 07/09/2018