Kununua dhahabu kwa njia ya kadi ya benki

Swali: Inajuzu kununua dhahabu kwa kadi ya benki?

Jibu: Dhahabu ikinunuliwa kwa pesa ya kawaida basi ni lazima kila mmoja achukue chake kabla hawajatengana. Mnunuzi achenchi pesa hizi na alipe kwa dirhamu na hivyo tatizo litakuwa limeondoka. Njia nyingine yule mnunuzi anaweza kuwasiliana na benki yake akawaomba watoe pesa kutoka benki yake na kuweka kwenye akaunti ya yule muuzaji. Hapo yule muuzaji atakuwa amempa dhahabu yule mnunuzi na amepokea pesa yake kwa njia ya kuwekewa ndani ya akaunti yake hali ya kuwa bado hawajatengana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1300
  • Imechapishwa: 19/10/2019