Kununua bidhaa kutoka kwa Raafidhwah


Swali 226: Mfanyabiashara fulani akitambulika kuwa ni Raafidhwhiy na kwamba bidhaa zake ni zenye kujulikana kati ya watu. Je, atahadharishwe kwa kujengea kwamba wasinunue kutoka kwake? Zipo bidhaa zinazojulikana sokoni na zinatambulika kwamba mwenye nazo ni Raafidhwiy. Je, watahadharishwe naye na wawaeleze wasinunue bidhaa hizi ili wasimsapoti na asiwe na sapoti?

Jibu: Hili ni jambo linahitaji kuangalia vizuri. Kununua kutoka kwa makafiri ni jambo linalojuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinunua kutoka kwa mayahudi. Alinunua kutoka kwao na akafa nguo yake ya vita ameiweka rehani kwa myahudi kwa ajili ya chakula cha familia yake[1]. Lakini kinachotakiwa ni kwamba wabainishiwe ´Aqiydah yao ili isije kufuatwa na jamaa wala marafiki. Ama kuhusu kununua kutoka kwao kitu, haja ikipelekea kufanya hivo ni jambo jepesi. Hata hivyo mtu asiwafanye kuwa ni marafiki, akala chakula chao na vichinjwa vyao vilivyoharamishwa.

Muulizaji: Si ni bora zaidi endapo mtu akanunua kutoka kwa wengine?

Jibu: Kinachokusudiwa ni kwamba mtu ajiepushe na kuwafanya marafiki, kuwapenda na kuchukulia wepesi pamoja nao. Watu wanapaswa kubainishiwa ukafiri na upotevu wao ya kwamba haya ni katika matendo yao. Wanamtukana as-Swiddiyq, wanamtukana ´Umar, wanawatukana Maswahabah wengine, wanawataka msaada watu wa kwa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanamtaka uokozi ´Aliy, matendo ambayo ni shirki kubwa. Kuwatukana Maswahabah ni kufuru yenye kujitegemea. Maana yake ni kwamba mtu anawafanya ni wenye khiyana na si wenye kustahiki kupokelewa kutoka kwao.

[1] al-Bukhaariy (2068) na Muslim (4090).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 469
  • Imechapishwa: 12/04/2020