Kunuia kisomo cha ndani ya swalah kuwa ni Ruqyah kwa maamuma


Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan kwa nisba ya Imamu ikiwa anasoma juu ya Jamaa´ah [ya msikitini] kwa nia ya Ruqyah ya Kishari´ah?

al-Fawzaan: Sijafahamu swali. Yaani anawasomea Jamaa´ah ndani ya swalah au nje ya swalah?

Muulizaji: Inavyodhihiri ni ndani ya swalah.

al-Fawzaan: Yaani anafanya kisomo cha ndani ya swalah kuwa ni Ruqyah?

Muulizaji: Hii ndio dhahiri ya swali.

Jibu: Hili halikusemwa na yeyote na halijafanywa na yeyote. Yaani anawasomea Jamaa´ah walio nyuma yake? Subhaan Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014