Kundi la Qaadiyaaniyyah ni kundi limetoka katika Uislamu

Swali: Katika mji wetu kuna baadhi ya watu wanalingania katika kundi la Qaadiyaaniyyah na wanaonelea kuwa kundi lao ni sahihi na wanamsifu muasisi wake. Tunataraji utubainishie uhakika wa kundi hili.

Jibu: Kundi hili Qaadiyaaniyyah ni kundi ambalo limetoka nje ya Mila ya Uislamu. Wanajinasibisha kwa mtu ambaye yasemekana anaitwa “Ghulaam Mirzaa Ahmad Qaadiyaaniy”. Ni watu ambao wana dini na I´itiqaad ambazo ni maalum. Wanatoka India katika mji unaoitwa Qaadiyaaniy. Kutokana na I´itiqaad zao mji huu ni mji unaoadhimishwa na wanaenda kuhiji huko. Ni makafiri katika makundi ya makafiri. Kama walivyosema hilo na kupitishwa na kundi la wanachuoni wa Fiqh na baraza la wanachuoni wakubwa na wengineo. Makusudio ni kwamba Qaadiyaaniyyah ni kundi la kikafiri katika makundi ya makafiri na sio katika makundi ya Uislamu. Wao wana dini, ´Ibaadah na I´itiqaad ambazo ni maalum. Na wana Ka´bah yao maalum ambapo wanaenda kuhiji India. Wao ni katika makundi ya makafiri na sio katika makundi ya Waislamu. Ni wajibu kutahadhari na kazi zao, imani zao na matendo yao. Tahadharini vilevile na kujiunga nao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com//Fatawa/ID/1463
  • Imechapishwa: 04/09/2020