Jama´aat-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Suruuriyyuun, Hizb-ut-Tahriyr na wanaoshirikiana nao – wote hao ni fitina, ni fitina mmepewa kwayo mtihani. Nyinyi mko katika njia [sahihi], na makundi haya yanataka kuwatoka katika njia [hiyo] na kuwapeleka katika njia za utata. Na atakayetoka katika njia sahihi na kwenda katika njia za utata basi kapotea isipokuwa Atapopenda Allaah. Hivyo simnasihi yeyote kushikamana na kundi lolote katika haya makundi.

Jamaa´at-ut-Tabliygh ufahamu wake si kama makundi mengine, lakini ni kundi la Kisufi. Huenda wakahalalisha kuomba badala ya Allaah, kufanya Twawaaf kwenye makaburi katika miji yao – yaani msingi wao. Hata kama walioko hapa katika mji huu [Saudi Arabia] na miji mingine hatuwatuhumu kwa hilo, lakini kundi wanalojinasibisha kwalo lina Shirki, na huenda wakawa hata na Shirki kubwa. Kwa hivyo hakuna anayedai kutoka nao.

Kisha mpangilio wa kutoka – kwa siku tatu, au miezi mitatu na kadhalika – mipangilio yote hii ni ya Bid´ah. Hayana asili. Kisha kuchukulia kuwa ni “kutoka katika njia ya Allaah” ni Bid´ah. Wakitoka kwa ajili ya kutafuta elimu, kupigana vita, kusaidia ndugu katika Uislamu, wakitoka kwa sababu za Kishari´ah safari yao itakuwa safari ya malipo. Kusema kwamba ni katika njia ya Allaah, hili twamuachia Allaah. Ama kutoka huku wakiita “katika njia ya Allaah” hili ni kosa. Na walioanzisha kundi hili ni watu katika wahindi wasiokuwa waarabu. Huenda hawakufahamu maana yake. Lakini nyinyi ndo mnawasaidia kwa nini mnawafuata? Badala ya nyinyi kuwaathiri wao ndo wanawaathiri, huu ni ujinga mkubwa. Nyinyi mko na uwezo wa kuwaongoza, kuwapa nasaha n.k., ni waarabu mliyosomo na mnafahamu. Mnajiwa na watu wasiofahamu kitu zaidi ya kujinasibisha [tu na Uislamu], wenye njia mbali mbali waabudu makaburi kisha wanawaathiri? Badala ya nyinyi kuwaathiri katika yale mliyomo, huu ni ujinga mkubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/ByDCVzk7GjA
  • Imechapishwa: 30/08/2020