Kunatangulizwa mikono au uso wakati wa Tayammum?

Swali: Kuna baadhi ya mapokezi yanayotanguliza kupangusa uso kabla ya vitanga vya mikono na baadhi ya mengine yanatanguliza vitanga vya mikono kabla ya uso. Ni yepi maoni yenye nguvu katika hayo?

Jibu: Baadhi ya mapokezi yanatanguliza uso kabla ya vitanga vya mikono na khaswa katika hadathi kubwa. Baadhi ya wanachuoni wengine wanaona kuwa mpangilio ni wajibu katika hadathi ndogo pasi na hadathi kubwa. Katika hadathi ndogo ni lazima kutanguliza uso kabla ya vitanga vya mikono. Katika baadhi ya mapokezi imekuja:

“Halafu akafuta uso wake.”

Hapa ni wakati wa hadathi kubwa. Wapo baadhi ya wanachuoni waliosema kuwa kitendo hicho ni kutoka katika baadhi ya mapokezi. Kinachokusudiwa ni kwamba uso unatanguliza kabla ya vitanga vya mikono na khaswa wakati wa hadathi ndogo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 15/02/2019