Kunasomwa Qunuut kwa ajili ya kuondosha maradhi ya mlipuko?

Je, kusomwe Qunuut kwa ajili ya maradhi ya mlipuko na tauni[1] au hapana? Ni ipi tofauti kati ya mawili hayo? Tauni ni kitu maalum zaidi kuliko maradhi ya mlipuko. Namna ilivyo ni kwamba husomwa Qunuut kwa ajili ya kuondosha maradhi ya mlipuko yasiyokuwa tauni na wala hakusomwi Qunuut kwa ajili ya kuondosha tauni kwa mujibu wa maoni yaliyochaguliwa na wanachuoni waliokuja baadaye. Kwa sababu kufa kwayo, bali katika wakati wake, ijapokuwa hakufa kwayo na bali katika wakati usiokuwa wake, mtu akibaki katika mji wake na siku zake hali ya kuwa ni mwenye kusubiri na mwenye kutarajia malipo kutoka kwa Allaah na hali ya kuwa ni mwenye kuridhia yatayomshukia, basi anakuwa ni shahidi. Hakuombwi du´aa kwa ajili ya kuondosha shahaadah kinyume na mwenye kufa kwa maradhi ya kawaida tu yaliyoenea. Mtu huyo hawi shahidi na hivyo imesuniwa kusoma Qunuut kwa ajili ya kuyaondosha.

[1] Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kuita maradhi ya tauni kuwa ni “maradhi ya mlipuko” (وباءً) haipelekei kwamba kila maradhi ya mlipuko ni tauni. Bali inafahamisha kinyume chake kwamba kila tauni ni maradhi ya mlipuko.

Lakini pale ilipokuwa kwamba maradhi ya mlipuko yanapelekea vifo vingi na vivyo hivyo ndivo inavofanya tauni, ndipo ikaitwa kwa msemo huo.” (Badhala al-Maa´uuna fiy fadhwl-it-Twaa´uun, uk. 104)

  • Mhusika: Haafidhw Ibn Hajar al-Haytamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Fiqhiyyat-il-Kubraa (01/141)
  • Imechapishwa: 05/04/2020