Kunasomwa Qunuut kwa ajili ya kuondosha maradhi ya mlipuko? II

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hasomi Qunuut isipokuwa anapowaombea watu du´aa nzuri au dhidi ya watu du´aa mbaya.

Ameisahihisha Ibn Khuzaymah.

Hadiyth inafahamisha kwamba pindi waislamu wanapoteremkiwa na janga lisilohusiana na mwanadamu, kama mfano wa maradhi ya mlipuko[1] (كالأوبئة), mafuriko na kutetemeka kwa ardhi, basi hasomi Qunuut. Kwa sababu mambo haya yalitokea kwa wingi katika uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hakuwa ni mwenye kusoma Qunuut kwa ajili ya mambo hayo. Muda wa kuwa sababu ilikuweko katika zama za Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hakukuweko kizuizi, basi kufanya jambo hilo ainakuwa ni Bid´ah.

 [1]Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuita maradhi ya tauni kuwa ni “maradhi ya mlipuko” (وباءً) haipelekei kwamba kila maradhi ya mlipuko ni tauni. Bali inafahamisha kinyume chake kwamba kila tauni ni maradhi ya mlipuko.

Lakini pale ilipokuwa kwamba maradhi ya mlipuko yanapelekea vifo vingi na vivyo hivyo ndivo inavofanya tauni, ndipo ikaitwa kwa msemo huo.” (Badhala al-Maa´uuna fiy fadhwl-it-Twaa´uun, uk. 104)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buluugh-ul-Maraam, uk. 76
  • Imechapishwa: 05/04/2020