Kuna wakati wa kupokelewa du´aa baada ya swalah za faradhi?

Swali: Ibn-ul-Qayyim ametaja katika “ad-Daa´ wa ad-Dawaa´” kwamba baada ya swalah za faradhi kuna wakati ambapo du´aa inakuwa ni yenye kupokelewa. Hayo yanakuwa vipi? Je, inakuwa baada ya nyuradi za Kishari´ah, baada ya Raatibah zake au lini?

Jibu: Mimi sijui haya katika Sunnah kwamba kuna du´aa baada ya swalah isipokuwa zile zilizofungamana na swalah kama kufanya Istighfaar mara tatu baada ya kutoa salamu. Kwa sababu zinafungamana na swalah. Kuhusu du´aa inakuwa kabla ya salamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaja Tashahhud akasema:

“Kisha achague katika du´aa anayotaka.”

Du´aa ilioko kati ya adhaana na Iqaamah ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba ni yenye uwezekano mkubwa wa kuitikiwa. Ni mamoja mtu anaiomba katika swalah ya Sunnah au baada ya swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1126
  • Imechapishwa: 29/04/2019