Kuna tofauti ipi kati ya Khawaarij wa kale na wa leo?


Swali: Ni ipi tofauti kati ya Khawaarij wa kale na wa Khawaarij wa leo?

Jibu: Hakuna tofauti yoyote kati yao ikiwa Khawaarij wa leo wako juu ya yale waliyokuwemo Khawaarij wa kale. Ni katika mambo ya Khawaarij wa kale kuwakufurisha wale wenye kufanya madhambi makubwa na kusema kuwa watabakizwa Motoni milele. Hivyo yule ambaye leo yuko juu ya mfumo wa Khawaarij wa kale ni kama wao na hakuna tofauti yoyote kati yao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda ”al-Hamalaat al-I´laaniyyah dhiwdd Hukkaam wa ´Ulamaa’ Bilaad-il-Haramayn”
  • Imechapishwa: 05/09/2020