Kuna siku maalum za kula katika safari?

Swali: Kuna siku maalum za kula katika safari?

Jibu: Hakuna siku maalum. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoufungua mji wa Makkah ilikuwa katika Ramadhaan siku ishirini zilizobaki na hakufunga mwezi uliobaki. Hayo yamesihi katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) katika yale yaliyopokea al-Bukhaariy. Baada ya hapo kukabaki ima siku tisa au kumi. Akabaki (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah siku ishirini na tisa akifupisha swalah na akila katika Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/133)
  • Imechapishwa: 21/06/2017