Kuna sampuli ngapi ya swawm?


Swali: Kuna aina ngapi za swawm?

Jibu: Kuna aina mbili. Moja imefaradhishwa na nyingine ni ya sunnah.

Swawm iliyofaradhishwa inaweza kuwa inatokamana na sababu, kama swawm ya kafara na nadhiri, na inaweza vilevile kuwa haina sababu, kama swawm ya Ramadhaan. Kufunga katika Ramadhaan ni wajibu kwa mujibu wa Shari´ah tangu hapo mwanzo. Kwa msemo mwingine, wajibu huu haukusababishwa na mtu mwenyewe.

Swawm ya sunnah imegawanyika sehemu mbili: iliyofungamanishwa na ambayo haikufungamanishwa.

Mfano wa swawm ya sunnah iliyofungamanishwa ni ile ya kufunga jumatatu na alkhamisi.

Mfano wa swawm ya sunnah ambayo haikufungamanishwa ni kufunga siku yoyote ile ya mwaka.

Hata hivyo kumekuja dalili zinazokataza mtu kukhusisha kufunga siku ya ijumaa. Hivyo haitakiwi kufunga siku ya ijumaa isipokuwa ikiwa kama mtu atafunga siku ya kabla au ya baada yake. Kumethibiti vilevile makatazo ya kufunga za ´Iyd mbili. Vivyo hivyo haijuzu kufunga siku za Tashriyq isipokuwa kwa yule hujaji ambaye ni wajibu kwake kuchinja lakini akawa hakujaaliwa kufanya hivo. Huyu atatakiwa kufunga siku za Tashriyq badala ya siku tatu za hajj.