Kuna mambo ya kijinga kwenye vitabu vya Rabiy´ al-Madkhaliy? – Ibn ´Uthaymiyn anajibu

Swali: Tunajua mengi kuhusu upetukaji mpaka wa Sayyid Qutwub. Lakini kuna kitu kimoja ambacho sikukisikia kutoka kwake, bali nilisikia kutoka kwa mwanafunzi mmoja na sijakinaika nacho. Nacho inahusiana na kwamba Sayyid Qutwub ni mmoja katika wale wanaokubaliana na kauli ya Wahdat-ul-Wujuud. Hii ni kufuru. Je, Sayyid Qutwub ni katika wale wanaoamini Wahdat-ul-Wujuud? Natarajia jawabu, Allaah Akujaza kheri.

Jibu: Nilisoma kidogo vitabu vya Sayyid Qutwub. Sijui hali yake. Lakini hata hivyo, kuna wanachuoni ambao wameandika kuhusu kitabu chake “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”. Wameandika makosa mengi kutoka kwenye Tafsiyr yake. Kwa mfano Shaykh ´Abdullaah ad-Duwaysh (Rahimahu Allaah) na ndugu yetu Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy ameandika makosa ya Sayyid Qutwub katika Tafsiyr yake na vitabu vingine. Kwa ajili hiyo yule anayetaka, anaweza kuvirudilia.

  • Mhusika: Imâm Muhammad bin Sâlih bin ´Uthaymîn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda ”Liqaa´ as-Shaykh Rabiy´ m´a ash-Shaykh Ibn ´Uthaymiyn hawl al-Manhaj
  • Imechapishwa: 05/07/2020