Kuna mambo ya kijinga kwenye vitabu vya Rabiy´ al-Madkhaliy? – al-Fawzaan anajibu

Kipindi cha mwisho kumejitokeza makundi mengi yanayojinasibisha na Da´wah na yanaenda chini ya uongozi maalum kwao. Kila kundi linajifanyia mfumo wao wenyewe, jambo ambalo linazalisha mfarakano, tofauti na ugomvi unaotokea kati ya makundi. Hili ni jambo ambalo linapingwa na Dini na linakataliwa na Kitabu na Sunnah. Wakati baadhi ya wanachuoni wanakataza njia hizi za kigeni ambazo wametumbukia ndani yake, baadhi ya ndugu wanaenda kinyume na kuwatetea. Miongoni mwa watetezi hawa ni muheshimiwa Shaykh ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. Hili linaonekana katika vitabu vyake vinavyochapishwa na kanda zinazosikilizwa pamoja na kwamba ndugu yake ameshamnasihi kuhusu hilo. Ukiongezea juu ya hilo akaanza pia kuwasema vibaya wanachuoni ambao hawakubaliani naye juu ya mambo yake. Akawasifu kwa maneno yasiyostahiki na hawakusalimika na hayo hata wale waalimu zake ambao walimsomesha. Muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy amesimama kidete na kumraddi katika kitabu hichi ambacho msomaji yuko nacho mbele yake kwa anwani “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahidah laa ´Asharaat”. Nimekisoma na nimekuta kuwa kimetimiza lengo na himdi zote ni Zake Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dibaji ya ”Jamaa´ah Waahidah, laa Jamaa´aat”
  • Imechapishwa: 05/07/2020