Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza yale yanayoitwa “Anaashiyd za Kiislamu”? Je, kuna hali ambazo hukumu inatofautiana kutokana na nyingine?

Jibu: Sisi tulisema, bado tunasema, tutazidi kukariri na wengine katika wanasihi wanasema kuwa hakuna Anaashiyd za Kiislamu. Ni kweli kuwa kuna Anaashiyd. Ama kuziita “za Kiislamu” si kweli. Kuna dalili ipi ya kwamba ni za Kiislamu? Ikiwa ni za Kiislamu ina maana zimo katika Uislamu. Katika hali hiyo kutahitajika dalili ya kwamba ni za Kiislamu. Ni kweli kuwa kuna Anaashiyd. Anaashiyd ni aina moja wapo ya nyimbo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (12) http://alfawzan.af.org.sa/node/2055
  • Imechapishwa: 17/02/2017