Kuna dhambi mwanamke kutumia rangi ya kucha?

Swali: Kuna dhambi kwa mwanamke kutumia rangi ya kucha inayotiwa katika kucha? Afanye nini wakati anapotawadha?

Jibu: Hatujui chochote juu ya hili. Lakini bora ni kutofanya hivo kwa sababu hakuna haja ya jambo hilo. Jengine ni kwamba inaweza kuzuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha. Kwa kuhitimisha ni kwamba bora ni kutofanya hivo na mtu atosheke na hina. Bora ni kushiamana na yale waliokuwa nayo watu wa mwanzo. Mwanamke akiitumia basi ni lazima aiondoshe wakati wa kutawadha. Kwa sababu kama tulivyotangulia kusema inazuia maji kufika kwenye ngozi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/48)
  • Imechapishwa: 06/08/2021