Swali: Je, kuna dalili katika Sunnah inayokataza ukubwa wa mahari?

Jibu: Kakataza ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) mahari makubwa. Bora zaidi mahari yawe madogo kwa kufuata Sunnah. Hakika ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) anasema:

“Hakuzidisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mahari ya mke wake wala mabanati zake zaidi ya dirhamu tano.” (Hadiyth hii imepokelewa na Muslim)

Uongofu bora ni uongofu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Atakayezidisha na akawa anaweza hilo hakuna ubaya. Kama alivyosema Allaah:

“Mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote.” (04:20)

Nukta muhimu:

”Na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali.” (04:20)

Ikiwa anaweza hakuna ubaya. Wala watu hawahukumiwi hukumu moja, fulani alitoa kiwango fulani nawe toa kiwango fulani. Fulani anaweza kuwa na uwezo, na huyu mwengine akawa hana uwezo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4750
  • Imechapishwa: 22/09/2020