Swali: Kuna mtu ana deni la Ramadhaan ambapo amemwingilia mke wake ilihali amefunga. Je, juu yake ana kafara au anatakiwa tu kulipa siku hiyo?

Jibu: Kafara sio wajibu katika swawm za kulipa. Ikiwa mtu analipa deni la Ramadhaan kisha akamjamii mke wake mchana wa Ramadhaan, anapata dhambi. Ni juu yake kutubia na afunge siku nyingine badala ya siku hii. Hana juu yake kafara. Kafara ni wajibu pindi mtu anapofanya jimaa katika mchana wa Ramadhaan kwa yule ambaye swawm ni wajibu juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (17)
  • Imechapishwa: 19/11/2017