Kumwangalia kwa uficho mwanamke ninayetaka kumuoa na kutumiana wachumba picha

Swali: Inajuzu kwangu kumwangalia mwanamke ambaye nataka kumuoa bila ya familia yake kujua? Kwa mfano amehudhuria kwa ndugu zangu nikamwangalia bila ya yeye na familia yake kujua kwa vile – kwa idhini ya Allaah – nina azma ya kumposa lakini hata hivyo bado sijamtolea mahari. Kilichopitika tu ni kuwa yeye na wazazi wake wameafiki kabla ya mimi mwenyewe binafsi kwenda kujitambulisha. Nimeswali swalah ya Istikhaarah. Je, kuangalia kwangu huku kunajuzu?

Jibu: Kuangalia kwako huku kunajuzu[1]. Mtu akiwa na azma ya kumuoa na mwaname na akawa na dhana yenye nguvu kuwa atakubaliwa, inafaa kwake kumtazama. Bali imesuniwa kwake kumtazama. Kwa sharti wasikae faragha na ajiamini kutotokea fitina. Ikiwa hatokuwa kukaa faragha na akaamini kutotokea fitina na akamwangalia yale yenye kutosha ambayo yanamvutia – kama kuangalia uso, kichwa, vitanga vya mikono na miguu – ni sawa. Bali ni katika mambo yaliyowekwa katika Shari´ah. Mambo haya ni salama zaidi kwa kuwadumisha wanandoa na kuwaunganisha.

Kuna watu wanauliza kama inajuzu kumuomba picha yake? Haijuzu.

Mosi: Picha inaweza kubaki mikononi mwa huyo mposaji hata kama atakataliwa.

Pili: Picha haiwakilishi uhalisia wa kweli. Picha aidha inaweza kumfanya kuonekana mbaya kama ambavyo vilevile inaweza kumfanya kuonekana mzuri. Matokeo yake mtu akadanganyika.

Tatu: Haifai kwa mtu kumwacha mwanaume akaangalia picha ya ahli zake; wasichana wake, dada zake na mfano wa hao. Bali hata kwake – yaani huyo mposaji – haijuzu kuiangalia kutokana na fitina inayopatikana kwa kufanya hivo na huenda vilevile picha hii ikaanguka mikononi mwa watu waovu na wakawaonyesha watu msichana wako. Hatimae msichana huyo akiwa mzuri inakuja kuwa ni fitina kwa watu. Na akiwa ni mbaya anakuja kusemwa vibaya.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/9-kumtazama-mwanamke-kwa-kujiiba-katika-mnasaba-wa-posa/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (22)
  • Imechapishwa: 30/12/2018