Kumwambia mtu “Shukurani za dhati”


Swali: Inajuzu kwa mtu kumwambia ambaye amemfanyia wema na anataka kumshukuru: “Shukurani za dhati.”?

Jibu: Mshukuru kwa kiasi cha wema:

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ

“Na Tumemuusia mwanaadamu wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake akimzidishia udhaifu juu ya udhaifu, na [kumnyonyesha] kuacha kwake ziwa katika miaka mwili ya kwamba: Unishukuru Mimi na wazazi wako – Kwangu ndio marejeo ya mwisho.” (23:14)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hamshukuru Allaah yule asiyewashukuru watu.”

Mshukuru kwa kiasi cha wema wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 29/04/2018