Swali: Maiti akifa na baada ya kumuogesha na kumvisha sanda wanakuja ndugu na marafiki zake kumsalimia na kumbusu. Je, kitendo hicho kina msingi katika Shari´ah?

Jibu: Hakuna ubaya. Ni aina fulani ya kumuaga na kumuombea du´aa. Hakuna neno. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokufa, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) aliingia ndani mwake, akamfunua uso wake na akambusu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 25/05/2019