Swali: Kuna ndugu mmoja amefurahi sana wakati aliposikia kuwa umekuja na akawa amekuja katika dawrah hii na akamwacha mke wake na yuko katika hali ya kutaka kuzaa. Je, kitendo chake hichi ni sahihi na anapata dhambi kwa kumwacha?
Jibu: Ikiwa yuko na ndugu wanawake au ndugu wanaume nyuma ya pazia, wanaomsimamia na ukamwachia pesa anazohitajia ni sawa. Allaah (´Azza wa Jalla) amesema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ
“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah.” (05:02)
Wanasaidiana katika wema na uchaji Allaah. Amekuja kwa ajili ya kutafuta elimu, kujifunza na anarudi – Allaah akitaka – kuwafundisha wao.
Na ikiwa hakuacha yeyote wa kumwangalia na hakuacha pesa anazohitajia, basi anapata madhambi. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah na kuomba msamaha.
  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=6689
  • Imechapishwa: 21/12/2020