Swali 225: Nikija na nikakuta safu imejaa – je, nimvute mtu pamoja nami au niswali peke yangu?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni wewe kubaki hali ya kusimama mpaka aje mtu. Asipokuja mtu basi umekwishaandikiwa kuswali mkusanyiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapokuja mmoja wenu msikitini na akawakuta watu wamekwishaswali, basi huandikiwa mkusanyiko.”

Ama Hadiyth ya kumvuta mtu ni dhaifu.

Kuhusu kuswali peke yako nyuma ya safu basi itambulike kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna swalah ya mtu mmoja nyuma ya safu.”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema akimwamrisha yule aliye nyuma ya safu airudi swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuunga safu basi Allaah atamuunga na mwenye kukata safu Allaah atamkata.”

Haijuzu kwa yeyote kukata safu kwa kumvuta mtu. Kinachompasa ni yeye kusimama mpaka aje mtu na ajiunge pamoja naye. Asipokuja mtu basi abaki hali ya kusimama kisha ndio aswali au atolewe swadaqah na mtu. Vinginevyo unaandikiwa kama umeswali mkusanyiko. Hakuna neno pia ikiwa ataenda kuswali upande wa kulia kwa imamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 441
  • Imechapishwa: 27/10/2019